Saturday, December 27, 2014

RANGERS MADISHI SITE UPANGA

Rangers Madishi leo tukiwa Upanga tukifanya kazi ya kufunga cable kwenye Apartment.


 Fundi akiwa anafanya kazi yake katika hali ya utulivu na umakini zaidi.

Karibu Rangers Madishi kwa huduma nzuri na safi za Digital & Satellite.

Friday, December 26, 2014

HIGHLAND VILLAS APARTMENT TUKIFUNGA DSTV

Rangers Madishi asubuhi ya leo tupo  HIGHLAND VILLAS APARTMENT tukifunga dishi za DSTV 6 katika apartment tofauti, na kazi ndivyo inavyoendelea sasa hivi.






  

  Kwa huduma nzuri na safi za Satellite  karibu RANGERS MADISHI.

RANGERS MADISHI POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA KWA WAKATI..!

 

Thursday, December 25, 2014

RANGERS MADISHI TUNAWATAKIA SIKUKUU NJEMA

Uongozi wa RANGERS MADISHI tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wadau na wateja kwa kuwa pamoja nasi toka tunaanza na mpaka sasa tunamaliza mwaka. Rangers Madishi tunashukuru sana na tunaahidi kuboresha huduma zetu katika kila sekta. Tunapenda kuwatakia sikukuu njema.



Saturday, December 13, 2014

AZAM TV MWENDO ULE ULE.

Azam tv ikiwa imejipanga vizuri katika kutoa burudani kwa wateja wake Leo tarehe 13/12/2014 itarusha matangazo yake live  kupitia Azam One mechi ya Mtani jembe kati ya Simba Vs Yanga. Mechi itaanza saa 10:00 kamili Alasiri.


Karibu Rangers Madishi.

RANGERS MADISHI POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA KWA WAKATI..!

Monday, December 1, 2014

CHANNEL YA ITV KUANZA LEO KWENYE KING'AMUZI CHA DSTV.

Ndugu mteja tunapenda kukujuza kwanzia leo mishale ya saa 5 Asubuhi channel ya ITV itaanza kufanya kazi katika king'amuzi chako cha Dstv. Itapatikana katika no 293. ITV DAIMA ndani ya Dstv.


Karibu Rangers Madishi uhudumiwe vizuri 

RANGERS MADISHI POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA...!

OFA OFA DSTV YENYE MFUMO WA HD KWA TSH 99,000.

Pata king'amuzi cha Dstv  HD kwa Tsh 99,000.



Kwa bei ya Tsh 99,000 utapata king'amuzi cha Dstv HD + HDMI cable + AV cable + Adapter + Dish pamoja na Ufundi.



Wahi sasa OFA bado inaendelea.




Karibu Rangers Madishi

RANGERS MADISHI POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA...!


Tuesday, November 25, 2014

AZAM TV YAZINDUA MTONYO CHAP CHAP NI MWEZI MZIMA WA WATU KUVUNA MAHELA.

Kampuni ya Azam tv leo imezindua promosheni ya kila mwaka iitwayo Mtonyo Chap Chap, Mtonyo Chap Chap inawapa fursa wateja wa Tv kurejesha thamani ya matumizi yao ya ving'amuzi vya kampuni hiyo. Ili kuingia katika droo hii ndugu mteja  unatakiwa kununua king'amuzi kipya cha Azam tv na kukiwekea malipo ya mwezi 1 na washindi 100 watakuwa wanapata zawadi kila siku.


RANGERS MADISHI POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA KWA WAKATI...!

Monday, November 24, 2014

BEI MPYA YA KING'AMUZI CHA STARTIMES KUTOKA Tsh 79,000 MPAKA Tsh 59,000

Ndugu mteja tunapenda kukujuza bei mpya ya king'amuzi cha STARTIMES kwa sasa ni Tsh 59,000 pamoja na mwezi mmoja wa kifurushi cha KILI. Furahia na STARTIMES kwa msimu huu wa sikukuu.


 Karibu Rangers Madishi

RANGERS MADISHI POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA...!

Saturday, November 22, 2014

DSTV / TANDALE

King'amuzi cha Dstv kikiwa kinaendelea kufanya vizuri katika mauzo nchini Tanzania, Ranger Madishi nasi tukifanya vizuri katika kuuza na kufunga dishi za DSTV katika hali ya usafi na yakupendeza.


Hatua inayofuata ni kufitisha stendi ya Dishi ukutani.


Dishi ipo tayari.


Karibu Rangers Madishi  uhudumiwe kwa wakati.

RANGER MADISHI POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA KWA WAKATI...!


DSTV / GONGOLAMBOTO (MAJOE)

Rangers Madishi tukiwa Gongolamboto tukifunga king'amuzi cha Dstv.


Baada ya kuliunganisha dishi tunafitisha stendi ya dishi ukutani katika hali ya usafi.



Sasa tunatafuta signal za DSTV.


Signal tayari tumeshazipata sasa tunaunganisha king'amuzi cha DSTV na Tv.


Furahia na endelea kufuatilia  vipindi vya DSTV.


Karibu Rangers Madishi upate huduma nzuri na safi


Karibu Rangers Madishi tupo kwajili yako.

RANGERS MADISHI POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA...




Wednesday, November 19, 2014

Je wajua Tv ikikaa ukutani inavyopendeza katika nyumba yako..?

Rangers Madishi tukiwa tunazidi kufanya vizuri katika kazi zetu za ufundi tupo Tegeta tukifunga Tv ukutani kwa mtindo wa kisasa katika hali ya usafi.

Tazama Tv muonekano wake wa mwanzo ilivyokua imewekwa chini.


Sasa kazi ndo inaanza kuifunga Tv ukutani. Ila kitu cha kwanza kabla ya kuifunga tv yako ukutani lazima uangalie upande upi ambao tv ikifungwa ukutani itapendeza zaidi na pia lazima uangalie sebule jinsi ilivyokaa. 

Hatua ya kwanza lazima upime stendi yako ukutani na kuweka alama kwajili ya kutoboa. Na zingatia sana stendi isiwe juu sana wala chini sana.


Tunaanza kutoboa matundu kwajili ya kufunga stendi
.

 Tv ipo ukutani

Hapo fundi anachukua vipimo kwajili ya namna atakavyozificha nyaya hizo zilizozagaa kwenye Ukuta.

Sasa tv ipo tayari 

Tazama sasa sebule inavyovutia.


Karibu Rangers Madishi ujipatie huduma nzuri na safi

RANGERS MADISHI POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA KWA WAKATI.!

Tuesday, November 18, 2014

Dstv MTONGANI KIJICHI

King'amuzi cha Dstv kikiwa kinaongoza kutoa huduma nzuri Rangers Madishi tupo Mtongani Kijichi tukifunga Dstv.


Hatua inqayofuata ni kuunganisha dishi pamoja na kulitafutia signal.

.

Sasa king'amuzi chetu cha Dstv kipo tayari kwa kuangalia.


Karibu Rangers Madishi hufurahie huduma zetu

RANGERS MADISHI POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA...!


Saturday, November 15, 2014

DAR MPAKA CHALINZE

Rangers Madishi tupo chalinze tukitathimini Ukumbi huu.



Ukumbi huu unatakiwa kufungwa Tv 6, pamoja na Projecta 4 


RANGERS MADISHI POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA...!

Friday, November 7, 2014

JINSI YA KUWEKA FLAT SCREEN UKUTANI BILA NYAYA KUONEKANA.

Hii limekuwa ni tatitzo kubwa miongoni mwetu, maana utakuta nyumba nzuri, sebule nzuri ila kwenye ukuta wa Tv nyaya kibao kiasi kwamba sasa inaharibu muonekano na kua kama uchafu.

Huu ndio muonekano wa Tv katika nyumba zetu.

Sasa kazi inaanza kuzipitisha nyaya za speaker kabla ya kuweka Flat ukutani.



Flat screen tayari ipo ukutani 


Na huu ndio muonekano wa Tv yako ambavyo tayari tumeshaingiza nyaya na hazionekani nyuma ya Tv yako.

Karibu Rangers Madishi ujipatie huduma safi kutoka kwetu. kwa mawasiliano wasiliana nasi kupitia no:0719 154554 / 0737 216792.


RANGERS MADISHI TUPO KWAJILI YAKO POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA.


Azam tv

Rangers Madishi tukiwa tunatokomeza dishi ambazo zimefungwa chini ya viwango. Tupo tandale tukihamisha dishi la Azam tv ambalo lilifungwa kwenye mbao zilizooza.


Hapo fundi akiwa anafunga standy kiumakini.




Fundi anaweka signal za Azam tv.


Karibu Rangers Madishi uhudumiwe vizuri  na gharama zetu ni nafuu.



RANGERS MADISHI TUPO KWAJILI YAKO POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA.

Dstv

Rangers Madishi tupo Salasala tukirekebisha Dishi la Dstv lililopoteza signal kutokana na sehemu iliyofungwa kutokuwa imara kuweza kuhimili kasi ya upepo na kusababisha kupoteza signal.


 Kazi inaanza kulifungua dishi kwajili ya kulihamishia sehemu sahihi.



Fundi akiwa anafunga vizuri standy kwajili ya kuliweka dishi na kulitafutia Signal.



Kazi imeshakamilika sasa kazi ni kwako ndugu mteja kufwatilia vipindi vizuri kutoka Dstv.


RANGERS MADISHI TUPO KWAJILI YAKO POPOTE ULIPO TUNAKUFIKIA 

Tuesday, November 4, 2014

Site Upanga Azam tv.

Rangers Madishi leo tupo Upanga kwenye jengo la Kushi Apartment ghorofa ya 10 tukifunga Azam tv.


Sasa kazi inaanza kuliunda dishi pamoja na kuliwekea signal.


Signal tayari zimeshapatikana imebaki kupitisha waya.


Hapo kazi imeshakamilika kazi kwako ndugu mteja kufurahia vipindi vya Azam tv.




Rangers Madishi tunatoa shukrani za dhati kwa Kushi Apartment group kwa ushirikiano ambao tuliokua nao kwanzia mwanzo wa kazi mpaka kuitimisha kazi.




Rangers Madishi tupo kwajili yako popote ulipo tunakufikia...!